Kampuni ya Startimes imeingia ubia na benki ya TPB kwa lengo la kuwakopesha wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao utamwezesha mteja kulipa mpaka miezi kumi na miwili kutoka benki ya TPB.
Ubia huu unamwezesha mteja wa startimes kulipia kwa njia rahisi zaidi televisheni ya kidigitali sio tu kwa mara moja bali kwa awamu kupitia Benki ya TPB, na wateja wataweza kuipata huduma hii katika mikoa mitano ambayo ni Dar es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na Mbeya ambapo kuna matawi ya Benki hiyo.
Akiongea katika uzinduzi, Meneja Mahusiano wa StarTimes, Bw.Antony Katunzi alisema, “Ushirikiano huu unaashiria wazi mapinduzi ambayo Benki na Kampuni ya Televisheni zinaweza kuleta, kwa kurahisisha ulipiaji kwa wateja wao na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kila familia kumiliki luninga ya kidigitali ya StarTimes”.
Naye Amos Kasanga, Meneja Masoko wa Benki ya TPB amesema benki hiyo imekubaliana na StarTimes kutoa mikopo hiyo midogo kwenye mikoa mitano ambapo huduma hiyo itapatikana. Njia hii ni rahisi zaidi kwa wateja kutumia.
“Najisikia furaha kubwa leo tunapozindua njia nyingine ambayo inazileta pamoja kampuni hizi kubwa mbili Tanzania, na hii itatoa fursa kwa wateja na kila familia ya kitanzania kumiliki luninga ya kidigitali na kufurahia maisha ya kidigitali kwa kupata vipindi mbali mbali kutoka kila kona ya dunia.”
Kwa hatua hii, wateja na wasio wateja wa StarTimes, wote wanaweza kulipia luninga za kidigitali za StarTimes kwa awamu kupitia matawi ya Benki ya TPB. Watanzania waishio mijini na vijijini sasa wataweza kumiliki luninga za kidigitali kwa urahisi, kulingana na mahitaji na uwezo wao kifedha.
Tunayo matoleo mbalimbali ya luninga za kidigitali kwa ajili ya wateja wetu kulingana na mahitaji na uwezo wao. Tuna luninga ya inchi 24 kwa Tsh. 45,000/=,kwa kila mwezi kwa miezi kumi na miwili (12),inchi 32 Tsh 64,000/= na inchi 40 kwa Tsh. 99,000/= .
0 COMMENTS:
Post a Comment