May 26, 2017
Mara tu baada ya winga wa Yanga, Simon Msuva kutwaa Tuzo ya Mfungaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu Bara 2016/17, akiwa amefungana kwa mabao sawa na mshambuliaji wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa, winga huyo ameibuka na kusema kwamba tuzo hiyo ataikabidhi kanisani kwake.

Msuva ambaye ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili baada ya msimu wa 2014/15 alipoibuka mfungaji bora akifikisha idadi ya mabao 17, amesema anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kutwaa tuzo hiyo kwa mara nyingine.

“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kutwaa tuzo hii kwa mara nyingine, hivyo natarajia Jumapili hii kuipeleka kwa mchungaji wangu wa kanisa ili waumini wenzangu pia waweze kuiona na kuniombea tena kwa pamoja kama walivyokuwa wakinifanyia hapo mwanzo kabla ya kutwaa tuzo.


“Nalazimika kufanya hivi kwa kuwa waumini na mchungaji wangu ndiyo sehemu yangu ya kwanza ya mafanikio yangu yote ya uwanjani, kwani wamekuwa wakiniombea mara kwa mara kiasi kwamba nakosa hata kitu cha kuwalipa kwa sala zao zaidi mimi nitaendelea kuwashukuru na kuwapelekea kila sehemu ya mafanikio ya kazi yangu ili na wao waone umuhimu wa maombi yao kwangu,” alisema Msuva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV