May 20, 2017

KARATASI HIZO IKIWEMO LISITI YA TRA ZINAONYESHA TAYARI SIMBA WAMEISHATUMA MALALAMIKO YAO FIFA.

Ushahidi kuwa klabu ya Simba imewasilisha malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), umepatikana.

Kitendo cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na picha ikionyesha ushahidi huo, inaonekana kuwakwaza zaidi ya mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wameanza sherehe za ubingwa.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwaita Simba “Wazee wa pointi za mezani”.

Lakini mashabiki wa Simba wamekuwa wakijibu mapigo na kusema, “Haki ni haki” na sheria itafuata mkondo wake.

Yanga na Simba zimemaliza ligi zikiwa na pointi 68 kila moja, lakini Yanga ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa GD.

Silaha ya Simba, inabaki kuwa suala la pointi za Kagera na kama kweli Fifa itaamuru irejeshewe, basi itafikisha pointi 71 na kutangazwa kuwa bingwa.

Simba ilishinda rufaa yake kupitia kamati ya Saa 72 ambayo ilibaini kuwa kweli beki Mohammed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano wakati Simba ilipolala kwa mabao 2-1 katika mechi ya ligi Kuu Bara.

Lakini Kagera Sugar ilikata rufaa katika kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji na kushinda ikarejeshewa pointi zake tatu.

Hata hivyo, wakati wa kutangaza kamati hiyo ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji haikutoa ufafanuzi wowote kuhusiana na Fakhi kama alikuwa na kadi mbili au tatu za njano.

Badala yake ikasema rufaa ya Simba ilichelewa pia haikulipiwa hivyo kuifanya iwe batili.

Lakini kuhusiana na pointi hizo tatu, inaonekana hata kama Simba isingekata rufaa na kama kweli Fakhi ana kadi tatu za njano, basi automaticaly, Kagera Sugar wangepokwa ushindi.


Hivyo, Simba imeamua kwenda Fifa kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama itafanikiwa, basi moja kwa moja inatangazwa kuwa bingwa.

6 COMMENTS:

  1. Akili ni muhimu ikatumika kwenye suala la simba kukosa ubingwa na ikumbukwe kuwa fifa hawawezi kufanyia kazi hoja za simba Bila kupata taarifa ya tff ambayo kimsingi ililidhia point zilejeshwe kagera sugar. Nishauri kuwa simba ijipange kwa ajili ya kombe la shirikisho na ligi ya vpl mwakani kwani rufaa yao fifa haitofuta ubingwa wa yanga Bali mara zote matukio kamahayo maamuzi yake huishia kwa klabu ama mchezaji kupigwa faini na sikubadili matokeo ya uwanjani. na si vizuri kuwaaminisha wapenzi wa simba juu ya simba kupata point za mezani toka fifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu naona unatoa maoni ukisukumwa na ushabiki. Subiri Fifa wafanye kazi yao

      Delete
    2. aaah we ndo fifa unajua nini kuhusu fifa?

      Delete
  2. kaka Cosmas,Kaa kimya na tulia usijifanye wewe ndio FIFA,acha FIFA watoe mahamuzi yao na si TFF au ww ambao ni wababaishaji.

    ReplyDelete
  3. Tff ni wababaishaji hawakutowa sababu za msingi. Eti wamewauluza mashabiki na kujibiwa hana kadi tatu.

    ReplyDelete
  4. unajua haki itabaki kuwa haki yako tu na kama sheria inafafanua vizuri inakuwaje unapindisha sheria pale tff kuna uyanga na usimba ila tutaona kincho fata baada ya hapo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic