May 19, 2017





Wafanyakazi wote wa DStv wavaa sare za Serengeti boys kama njia mojawapo ya kuwaunga mkono katika ushiriki wao katika michuano inayoendelea ya kombe la Afrika kwa wachezaji wa umri wa chini ya miaka 17 nchini Gabon.


Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya wafanyakazi hao wamesema kuwa kwakuwa DStv imejikita kwenye kuwapa wananchi burudani, na kwakuwa wanaonyesha michuano hiyo mubashara, wameona ni ni vyema wakawaunga mkono Serengeti boys kwa njia ya ziada – yaani kuvaa jezi zao kama kwa siku ambayo timu hiyo inacheza.


Wamesema wanatambua kuwa Serengeti boys inatuwakilisha hivyo ni muhimu sana kuinga mkono hata kwa kuishabikia tu hata kama hatupo uwanjani.


 “Tumeamua kuvaa sare za Serengeti boys leo kama ishara ya kuwaunga mkono na kuwatakia kila la heri katika michuano hii inayoendelea nchini Gabon” alisema Revina Bandihai na kuongeza kuwa wana imani na matumaini makubwa sana kwa Serengeti Boys kwani ni timu ambayo imeonyesha kiwango cha hali ya juu.



DStv inaonyesha mubashara michuano hiyo na mechezo yote ya Serengeti boys inarushwa kwenye Supersport Select inayopatikana kuanzia kufurushi cha DStv Bomba kw ash.19m975 tu ikiwa kwenye Lugha yetu pendwa ya Kiswahili.

Leo Serengeti Boys inacheza na Angola saa 11.15 jioni Supersport Select DStv chaneli namba 233.


#KilaDStvIlipoDStvTupo

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic