May 6, 2017


Tayari JKT Ruvu wamechungulia "kaburi" la kuteremka daraja baada ya kuchapwa kwa mabao 2-1 na Toto African.
Katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo. Wenyeji walipata mabao mawili ya harakaharaka.
Nahodha wa JKT, Frank Nchimbi, amesema bahati haikuwa yao na wana hali mbaya.
"Hatukutaka hii itokee na tulipambana sana. Lakini mambo hayajaenda vizuri.
"Hatuwezi kujua mbele kuna kuna, tutakachofanya ni kushinda mechi zetu mbili, halafu tutamuachia Mungu, yeye ataamua huko mbele,: alisema Nchimbi.

Baada ya kipigo cha leo, JKT inaendelea kubaki mkiani ikiwa na pointi 23, ndogo kuliko za timu nyingine yoyote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV