May 6, 2017Nahodha wa Prisons, Benjamini Asukile amesema pamoja na kufungwa na Yanga bado hawajakata tamaa na Prisons lazima itabaki Ligi Kuu Bara.

Yanga imeitwanga Prisons kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini DAr es Salaam, leo.

Asukile amesema wana imani kubwa ya kuibakiza Prisons na walitaka kuanza kampeni yao dhidi ya Yanga lakini mambo yakawa magumu.
“Kuna makosa tulifanya kipindi cha pili na Yanga wakaitumia nafasi hiyo. Lakini tutaendelea kupambana na imani yetu Prisons itabaki ligi kuu,” alisema.


Prisons ina pointi 31, lakini bado haina uhakika wa kubaki kwa kuwa timu mbili za Toto African na Majimaji zilizokuwa na pointi 26, kila moja imeshinda leo na kufikisha pointi 29 hivyo kusababisha presha zaidi kwa askari Magereza hao kutoka Mbeya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV