May 8, 2017



Bosi wa benchi la ufundi la Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon, ameweka bayana kwamba hatishwi na idadi kubwa ya mechi zilizobakia kwa upande wa wapinzani wao Yanga na badala yake yeye anaangalia kikosi chake jinsi kitakavyoendelea kupata ushindi kwenye mechi zao.

Omog jana alikiongoza kikosi chake kupata ushindi dhidi ya African Lyon na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kikiwa kimebakiza mechi mbili.

Yanga mpaka sasa wamebakisha mechi nne zenye dakika 360 ambazo ni mbili mbele ya Simba.

Kocha huyo amesema kuwa kwake wala hana neno na hali hiyo kwani anaamini Yanga wanaweza kupoteza pointi kwa kuwa mechi hizo walizobakiza, baadhi ni dhidi ya timu ambazo zinapigana kutoshuka daraja, hivyo hazitataka kufungwa kirahisi.

Yanga imebakiza mechi dhidi ya Kagera Sugar, Mbeya City, Toto na Mbao.

“Kuwa mbele ya Yanga kimichezo kwangu wala hakuna kitu kinachoniathiri kwa sababu nimekita mawazo yangu katika kushinda mechi zetu na siyo kumuangalia mpinzani wetu anafanya nini au kabakisha idadi ya mechi ngapi.

“Kuwa na mechi nyingi kwa sasa sidhani kama ndiyo watatwaa ubingwa kwa sababu timu nyingi zinapigania kutoshuka daraja sasa unapokutana nazo zinacheza kufa na kupona kuhakikisha kwamba huzifungi na jambo hilo ndilo linalonipa imani kuwa wapinzani wetu hawatatufikia,” alisema Omog.    


3 COMMENTS:

  1. Mwambieni Omog hii ni Bongo timu inashuka daraja na wachezaji wanashangilia. Asishangae Toto atafungwa na Yanga na wachezaji wa Toto wakashangilia.

    Uzembe wake wa kushindwa kulinda tofauti ya point 8 mpaka kufikia kuiombea mabaya Yanga.

    ReplyDelete
  2. Mwambieni Omog hii ni Bongo timu inashuka daraja na wachezaji wanashangilia. Asishangae Toto atafungwa na Yanga na wachezaji wa Toto wakashangilia.

    Uzembe wake wa kushindwa kulinda tofauti ya point 8 mpaka kufikia kuiombea mabaya Yanga.

    ReplyDelete
  3. Mwambieni Omog hii ni Bongo timu inashuka daraja na wachezaji wanashangilia. Asishangae Toto atafungwa na Yanga na wachezaji wa Toto wakashangilia.

    Uzembe wake wa kushindwa kulinda tofauti ya point 8 mpaka kufikia kuiombea mabaya Yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic