May 17, 2017
Hatimaye kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu kongwe nchini ya Yanga.

Mkataba huo utakuwa ni wa miaka mitano na utagharimu kitita cha Sh bilioni 5.173 huku mwaka wa kwanza Yanga ikiingiza Sh milioni 950.

Mkataba huo umesainiwa hivi punde katika makao makuu ya klabu ya Yanga mbele ya waandishi wa habari.


Yanga inakuwa klabu ya pili kusaini mkataba na SportPesa baada ya Simba.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV