June 24, 2017



Mashabiki 4,000 wanatarajiwa kuingia bure kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 13, mwaka huu kutazama mechi ya kirafiki kati ya Everton ya England na Gor Mahia ya Kenya.

Gor Mahia imepata nafasi hiyo ya kucheza na Everton baada ya kutwaa ubingwa wa SportPesa Super Cup mapema mwezi huu.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba, wateja wao pekee wanaocheza michezo ya kubashiri matokeo ndiyo watakaohusika na ofa hiyo.

Alisema Everton itafika nchini Julai 12, mwaka huu na siku hiyo wataenda kutoa somo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa wanafunzi wanaosomea michezo.

“Tutatoa tiketi 4000 kwa ajili ya kuingia uwanjani kuishuhudia Everton ikicheza na Gor Mahia, hizi tiketi zitawahusu wateja wetu wanaobashiri michezo kupitia kampuni yetu.

“Hivyo, basi wateja wetu wanachotakiwa ni kuendelea kucheza mchezo wetu wa kubashiri matokeo ili wapate nafasi ya kuingia bure uwanjani, na tutawapa fulana maalum watakazovaa uwanjani,” alisema Tarimba.

Katika hatua nyingine, Tarimba alisema katika kukuza utalii nchini, Everton itavaa jezi zenye ujumbe wa kuisifia Tanzania na vivutio vyake kabla ya mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic