Mashabiki Simba bado hawajatulia hadi watakaposikia mshambuliaji Emmanuel Okwi atakapotua nchini leo.
Wengi wamekuwa akitaka kujua ni muda gani lakini taarifa zinaeleza ni leo jioni au usiku na Simba sasa wameamua kufanya siri kubwa.
“Okwi anakuja kesho na mambo yakienda vizuri atasaini mkataba wa kuichezea Simba kwa msimu ujao, kama hakuna kitu kipya kutoka kwake ni wazi atakuwa mchezaji wetu,” alisema mmoja wa mabosi wa Kamati ya Usajili ya Simba.
Simba tayari imeandaa jezi ya kumkabidhi Okwi muda mfupi baada ya kusaini mkataba wake muda wowote kuanzia atakapowasili nchini.
Okwi anarudi tena Simba akitokea SC Villa ambayo amemaliza nayo mkataba, hivyo kuna asilimia kubwa kwake akasaini kuichezea Simba.
Hata hivyo, kuna taarifa kwamba Okwi anatakiwa na timu moja ya Zambia ambayo inataka kumtumia kwa msimu ujao wa ligi na dili hilo likishindikana ndipo anapoweza kujiunga na Simba.
Pia imeelezwa, kama Simba ikishindwa kumtimizia Okwi mambo yake ya usajili anaweza kuendelea na dili lake la timu ya Zambia.
0 COMMENTS:
Post a Comment