June 22, 2017
CEO wa klabu ya Everton ya Robert Elstone, amesema ujio wao nchini utawasaidia kujifunza mengi.

Everton itashuka dimbani Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam kucheza dhidi ya Gor Mahia ambao ni mabingwa wa SportPesa Super Cup.
Elston amesema ana imani watajifunza kwa kuwa ni mara ya kwanza wanafanya ziara Afrika tena katika kipindi cha maandalizi ya Ligi Kuu England.

“Maandalizi ya ligi si kitu cha mzaha hata kidogo. Lakini timu itakuwa Tanzania na tunaonyesha si jambo dogo.

“Baada ya mechi hiyo dhidi ya mabingwa wa Super Cup, tutaondoka kwenda kuendelea na maandalizi mengine.

“Kikubwa ambacho tunaamini ni kwamba tutajifunza mambo mengi na tungependa kuona mambo yanabadilika kwamba unaweza kwenda Afrika na kufanya maandalizi bora,” alisema.
Elstone amesema, watatua nchini wakiwa na kikosi kambili pamoja na wachezaji ambao watakuwa wamejiunga na kikosi hicho.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV