June 22, 2017


Mashabiki wa Arsenal wameonekana kushitushwa na jezi namba 7 za msimu ujao ambayo inawaonyesha kuwa mshambuliaji wao Alexis Sanchez, ameishaagana nao.

Arsenal imetangaza jezi mpya, lakini kinachoonyesha kuwashangaza ni kwamba katika jezi hizo, yenye namba 7 imeandikwa jina la Welbeck badala ya Sanchez.

Wakati masabiki walipoanza kununua jezi hizo kwa pauni 77, takribani Sh 280,000 wamekuwa wakishangazwa na hilo.


Hata hivyo, Arsenal bado haijatangaza rasmi kama Sanchez anaondoka au amebadilishiwa jezi tu. Tayari raia huyo wa Chile alishaonyesha kwamba amenuia kuondoka na Bayern Munich na Chelsea zilikuwa kati ya timu zinazomuania kwa udi na uvumba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV