June 14, 2017Beki mtata wa kati, Juma Nyosso ataanza kuonekana tena katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Nyosso amejiunga na Kagera Sugar kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja. Sasa atakuwa chini ya Kocha Mecky Maxime.

Nyosso anaungana na wachezaji wengine kama Juma Kaseja aliyewahi kucheza naye Simba, pia ataungana na Mohamed Fakhi kuimarisha ukuta wa Wana Nkurukumbi.

Beki huyo mara ya mwisho aliitumikia Mbeya City, lakini akajikuta akifungiwa baada ya kumpapasa makalio Elius Maguri wakati huo akiwa Simba.

Sasa adhabu yake imefikia mwisho, naye anaamua kuibukia Kagera.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV