June 28, 2017
Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ni kati ya watu waliohojiwa leo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Kaburu ambaye ni mmoja wa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alionekana akiwa kwenye ofisi za makao makuu ya Takukuru leo wakati Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wa TFF, Mwesigwa Celestine walipokuwa wakihojiwa.

Hata hivyo Takukuru waliwazugumzia Malinzi na Mwesigwa pekee ambao walikiri kwamba walikuwa wakiwahoji.


Taarifa za ndani zinaeleza Malinzi na Mwesigwa wanahojiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi pia utakatishaji wa fedha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV