June 21, 2017
Beki mpya wa Yanga, Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’, amefichua siri kwamba, kiungo wa timu hiyo, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko amemtibulia katika suala zima la jezi aliyokuwa akiihitaji kuivaa muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga.

Ninja ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Yanga, akitokea Taifa Jang’ombe ya Zanzibar, amekabidhiwa jezi namba sita ambayo ilikuwa ikitumiwa na Mnyarwanda, Mbuyu Twite.

Beki huyo anayetajwa kuwa ndiye mrithi wa nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema chaguo lake la kwanza katika masuala ya jezi ni namba 13 ambayo amekuta ikitumiwa na Kamusoko.

“Binafsi napenda kuvaa jezi namba 13, hiyo jezi nimekuwa nikiipenda tangu zamani kwa sababu kuna shabiki wangu mmoja wakati najiunga na Taifa Jang'ombe aliwahi kuniambia huwa anapenda anione nikiitumia, kwa kuwa namkubali nikaona niitumie na nimekuwa nikiipenda sana.

“Nimekuja Yanga wamenipa jezi namba sita kutokana na ile niliyokuwa naipenda kuwa na mtu, sikuwa na jinsi kwa sababu naamini hata hii haiwezi kuniharibia kitu kwenye malengo yangu ndani ya Yanga ingawa ningepata ninayotaka ingekuwa vizuri,” alisema Ninja.
Tshabalala achimba mkwara mzito Simba
Ibrahim Mussa


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV