June 7, 2017



 LEBRON James na Stephen Curry, wote hivi sasa wapo mzigoni wakiendelea kuzitumikia timu zao katika vita ya kuwania ubingwa wa Ligi ya NBA msimu huu. LeBron msimu uliopita aliiongoza timu yake ya Cleveland Cavaliers, maarufu kwa jina la Cavs, kubeba ubingwa huo mbele y a Golden State Warriors ambapo m s i m u huu tena wamekutana katika fainali huku Curry akiwa ameshaiongoza Golden State kuongoza 2-0 hadi sasa. Hii ni mara ya tatu mfululizo timu hizo zinakutana katika fainali ya NBA (2015, 2016 na 2017) huku kila moja ikiwa imeshinda fainali moja. Ukiwauliza mashabiki ni nani mkali kati ya wababe hao, unaweza kupata maoni tofauti. Wengi wamekuwa wakijiuliza nani ni bora zaidi kati ya wakali hao wawili.  
Kupata ukweli wa hilo, ni takwimu pekee ndizo zinazoweza kuzungumza lugha ya ukweli zaidi, maana siku zote takwimu hazidanganyi, na katika michezo takwimu ndiyo kipimo kizuri cha kuaminika. Kwa kawaida, ukitaka kuwalinganisha mastaa wa kikapu, ni lazima utaangalia idadi ya mataji waliyotwaa, tuzo binafsi, takwimu za regular season na za playoff s.  
Maswali ambayo unaweza kujiuliza ni nani ambaye kafunga pointi nyingi katika maisha yake ya kikapu? Nani kafunga pointi nyingi kwenye playoff s? Nani ametwaa ubingwa mara nyingi zaidi? Nani aliongoza msimu mara nyingi zaidi? Nani ameshinda tuzo ya MVP (yaani mchezaji bora wa msimu) mara nyingi zaidi? Maswali hayo na mengine mengi, yatajibiwa hapa katika makala haya, ikiwa ni pamoja na anayeongoza kwa mipira iliyorudi, kwa maana ya rebounds, asisti na blocks. UBINGWA WA NBA: Curry ametwaa ubingwa huo mara moja, alipoiongoza timu yake ya Golden State kushinda taji hilo mwaka 2015, wakati LebRon amebeba ubingwa huo mara tatu: 2012 na 2013 akiwa na Miami Heat, pamoja na 2016 akiwa na Cavs.

MISIMU YA NBA: Curry ana misimu nane ya NBA akiwa na timu moja ya Golden State, wakati LeBron ana misimu 14 akiwa na Miami pamoja na Cavs. 
  KUCHEZA PLAYOFFS: Curry kacheza playoff s katika misimu mitano, wakati LeBron kacheza misimu 12. MVP: Curry amekuwa MVP mara mbili mwaka 2015 na 2016, wakati LeBron amekuwa MVP mara nne (2009, 2010, 2012 na 2013). 
  MVP WA FAINALI: Curry hajafanikiwa hata mara moja kuwa MVP wa fainali, wakati LebRon amefanikiwa mara tatu, mwaka 2012, 2013 na 2016. 
  MCHEZAJI BORA MWAKA WAKE WA KWANZA: Hii tuzo inajulikana kama Rookie of the Year, ikiwa na maana ya mchezaji bora katika mwaka wake wa kwanza NBA ambapo Curry hajawahi kuipata huku LeBron akiwa ameipata mara moja mwaka 2004.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic