June 23, 2017



Aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassani Dalali ‘Trump’, ametamka kuwa kama uongozi wa timu hiyo ukifanikiwa kumsainisha mkataba kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima basi wamekwisha.

Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache baada ya taarifa kuenea kuwa kiungo huyo amemalizana na Simba asilimia 80 kwenye mazungumzo yao kwa ajili ya kuja kukipiga Msimbazi.

Akizungumza na Gloabl TV Online kupitia kipindi cha Spoti Hausi, Dalali alisema Niyonzima ni kati ya viungo bora Afrika, hivyo anaamini kama akitua kuichezea Simba, basi msimu ujao wa Ligi Kuu Bara watakuwa na kikosi imara.

Dalali alisema anafurahishwa na uwezo wake mkubwa wa kuchezesha timu na kupiga pasi za mabao, hivyo ujio wake utaimarisha kikosi hicho kinachonolewa na Mcameroon, Joseph Omog.

“Ninasikia na kuona kwenye mitandao taarifa za viongozi wa Simba kuwa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kukamilisha usajili wa Niyonzima.

“Huyo ni kati ya viungo bora ninaowapenda na ninakumbuka kipindi cha uongozi wangu tulishawahi kumuhitaji kipindi hicho bado mdogo damu ikiwa bado inachemka,” alisema Dalali.


Kutazama mahojiano hayo zaidi tembelea Global TV Online kwenye mtandao wa YouTube.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic