June 23, 2017



Uongozi wa Yanga umempigia simu kiungo wake mshambuliaji, Deus Kaseke ukimtaka arejee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo.

Kiungo huyo, ni kati ya wachezaji 13 ambao mikataba yao imemalizika mwishoni mwa msimu uliopita akiwemo Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Vincent Bossou na Haruna Niyonzima anayetarajiwa kumwaga wino wakati wowote Simba.

Awali, kiungo huyo ilidaiwa kufuatwa na viongozi wa Simba kwa ajili ya kumpa mkataba wa kuichezea timu hiyo kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa za uhakika ni kuwa kiungo huyo anatarajiwa kutua Dar, leo kwa ndege akitokea nyumbani kwao Mbeya alipokwenda kwa ajili ya mapumziko mara baada ya ligi kuu kumalizika.

“Uongozi umeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika na kikubwa wanataka kuwaongezea mikataba mipya ya kuichezea timu hiyo.

“Miongoni mwa wachezaji hao ni Kaseke ambaye tayari uongozi umempigia simu na kumuita Dar ili asaini aongeze mkataba na kesho (leo) anatarajiwa kutua Dar kwa ndege kwa ajili ya kukamirisha usajili wake,” alisema mtoa taarifa.

Alipotafutwa Kaseke kuzungumzia hilo alisema: “Hizo taarifa za kweli, viongozi wameniita kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine mpya wa kuendelea kuichezea timu yangu hiyo na ndani ya wiki hii nitakuwa tayari nimefika Dar.”


Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema: “Uongozi hivi sasa upo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji tunaowahitaji ambao mikataba yao imemalizika, hivyo ni vema mkasubiria hadi tutakapokamilisha tutaweka wazi.” 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic