June 20, 2017Hiki ni kipindi cha majonzi ingawa kazi ya Mungu haina makosa.

Mashabiki au wapenda soka kwa umoja wao wameonyesha kuguswa na kifo cha shabiki maarufu wa soka nchini, Ally Yanga.

Ally Yanga amefariki dunia leo huko Mpwapwa baada ya kutokea kwa ajali mbaya ya gari.

Ajali hiyo mkoani Dodoma imechukua uhai wa shabiki huyo maarufu wa Yanga na mashabiki wa klabu hiyo, watani wao Simba na wapenda soka kwa ujumla wameonyesha kuumizwa.

Wengi wamekuwa wakiandika ujumbe mzuri kuwaliwaza Yanga ambao msiba unawahusu kwa kuwa ni shabiki wao.

Lakini wengi hawajasita kuonyesha kuwa msiba huo wa Ally Yanga ni wa taifa na wapenda michezo wote.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV