June 20, 2017


WAPENDA soka nchini watakuwa mashabiki wa kwanza wa soka kuwaona wachezaji wapya wa Everton wakiichezea timu yao kwa mara ya kwanza.

Ziara ya Everton nchini imeandaliwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambao ndiyo wadhamini wao wakuu wapya.

Everton itakuja nchini kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia na mechi hiyo itapigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tayari Everton imeshazinasa saini za nyota wawili akiwemo kipa Jordan Pickford kutoka Sunderland kwa dau la paundi milioni 30 ambalo limevunja rekodi ya usajili kwa magolikipa wenye uraia wa Uingereza.

Sambamba na Pickford, Everton pia wamemsajili kiungo na nahodha wa Ajax, Davy Klaassen kwa dau la paundi milioni 24.


Wachezaji wote hawa wawili watacheza mechi yao ya kwanza wakiwa kama wachezaji wa Everton kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam hivyo bila shaka hiyo itakuwa ni mechi yao ya kukumbukwa katika maisha yao ya soka ndani ya klabu ya Everton.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV