June 22, 2017
Mashabiki wa Yanga wameonyesha hasira zao kwa kuchoma moto jezi ya Haruna Niyonzima.

Mashabiki hao wa Yanga wameonyesha kuchukizwa na uamuzi wa Niyonzima kutosaini mkataba Yanga baada ya kushindwana na uongozi wa klabu hiyo.

Niyonzima ameamua kwenda Simba baada ya uongozi wa Yanga kushindwa kuongeza mkataba kutokana na kutokuwa na dau la kutosha.

Jana mchana, uongozi wa Yanga kupitia katibu wake mkuu, Charles Boniface Mkwasa ulitangaza kumuacha Niyonzima kwenda anakohitaji baada ya mkataba wake kwisha.

Yanga imesisitiza, imempa Niyonzima mkono wa kheri kwa kuwa haina uwezo wa kumsajiri tena.


Mashabiki hao wanaoelezwa kuwa ni wa Dar es Salaam, wamesikika wakipongezana kutokana na uamuzi wao wa kushoma jezi hizo namba 8 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Niyonzima aliyeichezea Yanga kwa miaka sita.

1 COMMENTS:

  1. Wanatokwa mapovu ya nn watulie..mbona wamemsajili ajibu ss hatujareact... Hii inaitwa jaza ujazweee .. walete mapovu ss tufulie....

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV