Singida United bado haijakamilisha usajili wake na inaelezwa kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ni kati ya watu wanaotakiwa na Kocha Hans van der Pluijm.
Habari kutoka ndani ya Singida United zinaeleza kuwa, Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm ameondoka kurejea kwake nchini Ghana, lakini amesisitiza kama akipatika Mkude, litakuwa jambo zuri.
“Kweli kocha amesisitiza kama kuna uwezekano. Tuna kiungo mpya mkabaji, lakini yeye ameendelea kumtaka Mkude.
“Kama itashindikana inaonekana halitakuwa jambo baya lakini pia ni kuhusu Ibrahim Ajibu. Naye akiwa anaweza kujiunga nasi pia ni kati ya wachezaji wanaohitajika,” kilieleza chanzo hicho.
Kumekuwa na taarifa pia kwamba wachezaji hao hasa Ajibu ana mazungumza na Yanga. Lakini Simba pia wamesema kimazungumzo walishamalizana naye.
0 COMMENTS:
Post a Comment