June 14, 2017


Simba imeendelea na usajili mfululizo baada ya kumtwaa kipa namba mbili wa Mbao FC.


Emmanuel Elias Mseja amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba.

Maana yake Mseja ni kipa wa pili kusajiliwa na Simba ndani ya mwezi mmoja.

Ilianza kumsajili Aishi Manula kutoka Azam FC ambaye kwa sasa ndiye kipa mwenye ubora wa juu kuliko wengine Tanzania.

Lakini tayari Simba ina makipa wawili, Denis Richard, Peter Manyika ambao ni Watanzania.

Hata hivyo, kusajiliwa kwa Mseja maana yake safari imemkuta Daniel Agyei raia wa Ghana kama ambavyo SALEHJEMBE iliwahi kuandika kuwa ametemwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV