June 7, 2017


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linaamini kikosi cha Taifa Stars kiko vizuri tayari kuimaliza Lesotho.

Stars imerejea nchini leo baada ya kambi ya nchini Misri tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi Saa mbili usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas aliyeongozana na kikosi cha Stars amesema maandalizi yalikuwa mazuri.

“Maandalizi chini ya Kocha Mayanga na wenzake yalikuwa mazuri na yenye mpangikio bora.


“Tunaamini kabisa kila kitu kimekwenda vizuri na kinachotakiwa ni kumalizia tu siku chache zilizobaki tukiwa hapa nyumbani,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV