June 7, 2017

Mchezaji bora zaidi katika mpira wa kikapu kuwa ni LeBron James wa Cleveland Cavaliers. 

NA SALEH ALLY 
KWA sasa hakuna ubishi mchezaji bora zaidi katika mpira wa kikapu kuwa ni LeBron James wa Cleveland Cavaliers. Katika fainali za NBA za msimu uliopita, LeBron alifanya kazi ya ziada kuiongoza Cavaliers kuibuka mabingwa dhidi ya kikosi cha Golden State Warriors kilichokuwa kinapewa nafasi kubwa.  
LeBron akabadili mambo na kuweka rekodi kibao huku akiwa amefunga pointi nyingi na kutoa pasi ny- ingi zaidi zilizoitengeneza timu hiyo na kuwa bora katika ushambulizi.  
Katika fainali za msimu huu, kwa mara nyingine Cavaliers wanakutana tena na Warriors na tayari zimeshachezwa mechi mbili, zote Cavaliers wamepoteza na kufanya matokeo hadi sasa kuwa 2-0. Cavaliers wanaendelea kubaki na LeBron lakini Warriors wao wanajivunia Stephen Curry ambaye walikuwa naye msimu uliopita kwa kuwa ndiye nyota wao. Mgeni katika Golden State ni Kevin Durant ambaye mashabiki wengi wa mpira wa kikapu wanapenda kumuita KD. Durant alikuwa katika kikosi cha Oklahoma City Thunders pamoja na Mtanzania Hasheem Thabeet. Mwisho amekuwa ndiye tegemeo wa kikosi hicho kabla ya kuhamia Warriors. Mashabiki wa Warriors wanaposikia Durant ni majeruhi au mgonjwa, hofu inatawala.  
Hii inatokana na mchango ambao ameuonyesha na umezaa imani kubwa wa mchango wake unafanya W a r r i o r s waamini Curry peke yake bila ya yeye mambo yatakuwa magumu. Hivyo nguvu ya Curry sasa inaegemea kwake na amegeuka kuwa dereva wa timu kwa kuthibitisha ubora wake. Katika mechi ya pili dhidi ya Cavs, Durant aliiongoza timu yake kushinda kwa pointi 132113, lakini mchango wake ulikuwa mkubwa zaidi katika kuendesha timu, kuzuia na kufunga. Takwimu zinaonyesha alicheza dakika 41 ambazo ni nyingi, akatoa asisti 6, akablock mara 5, rebaundi 13 na kufunga pointi 33. Mechi ya kwanza dhidi ya Cavs, katika block, rebaundi na asisti hakuwa mzuri sana lakini alifunga pointi 38 na kuendelea kuonyesha ni msaada zaidi. Uwezo wake huo umefanya apenye katikati ya LeBron na Curry ambao walikuwa gumzo zaidi na kila mmoja akijaribu kuangalia nani atakuwa mchezaji bora zaidi wa NBA.   Sasa anaanza kupewa nafasi kubwa ya MVP kumvuka Curry akionekana anaweza kuchukua nafasi ya LeBron ambaye katika mechi hiyo ya usiku wa kuamkia juzi alifunga pointi 29, rebaundi 11, asisti 14, ‘aliiba’ au steel mara tatu. 

Durant amekuwa ‘mtamu’ kitambo tu lakini hakuwa katika timu yenye wachezaji wenye mawazo ya ubingwa na ukweli sasa yeye na Cury wanategemeana. Kama watashinda mechi ya tatu mfululizo na yeye akaonekana tena ndiye dereva wa mchezo, basi itakuwa haina ujanja tena kumzuia kuwa kucheza na wachezaji kama Curry, Draymond G r e e n na Klay Thompson kunazidi kumfanya awe “on fi re” zaidi na huenda MVP imeanza kunukia. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic