June 20, 2017
Victor Wanyama amesema zaidi anazijua Yanga, Simba na Azam FC linapozungumziwa soka nchini.

Kiungo huyo nyota wa Tottenham Hotspurs ya England ametua nchini akiongozana na ndugu zake.

Wanyama yuko nchini kwa mapumziko na amesema anajua soka ya Tanzania, sawa na Kenya lakini timu hizo tatu ndizo anazozijua zaidi.

"Nazijua Yanga, Simba pia Azam FC. Soka la Kenya na Tanzania hakuna tofauti kubwa.

"Watu wa Afrika Mashariki tunapaswa kuungana na kusaidia maendeleo kwa ujumla," alisema Wanyama.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV