Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza kuifutia Zanzibar unachama iliyoutoa kwake, lakini siku chache baadaye, bendera ya shirikisho hilo, haijulikani ilipo visiwani humo.
Bendera iliyokuwa mbele ya ofisi za Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), imetolewa na inaelezwa imeshushwa lakini kila ofisa, anasema hajui ilipo!
Tangu ilipotangazwa Zanzibar imepata uanachama wa Caf Machi 16, mwaka huu, bendera ya Caf ilikuwa ikipepea katika Uwanja wa Amaan sehemu ya VIP nje kwenye bustani ndogo, hiyo ilikuwa ni kuashiria ya kuwa Zanzibar ni mwanachama wa kudumu namba 55 wa Caf.
Uamuzi wa kufutiwa uanachama ulitolewa Ijumaa iliyopita nchini Morocco wakati Kamati ya Utendaji ya Caf ilipokutana huku Rais wa ZFA, Ravia Idarous Faina, Katibu Mkuu wa ZFA, Mohd Ali Hilali ‘Tedy’ na Kocha wa Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman ‘Morocco’ nao wakiwepo.
Tamko hilo la kuondolewa uanachama limekuja wakati Hatua ya Nane Bora ya Ligi Kuu ya Zanzibar ikiendelea ambapo baadhi ya mashabiki wameanza kukata tamaa ya kufika uwanjani kutokana na majonzi yanayoendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment