July 24, 2017



Pamoja na klabu nyingi za Ligi Kuu Bara kufanya usajili makini kwa ajili ya msimu ujao, lakini Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ameibuka na kusema kuwa karata yake ameitupa kwenye kikosi cha Simba katika msimu wa 2017/18.

Simba ambayo msimu ujao watashiriki Kombe la Shirikisho Afrika, wamesajili nyota 12 kuelekea msimu huo kiasi cha kuwa gumzo katika dirisha hili la usajili.

Kifaru amesema kutokana na Simba kusajili wachezaji wazuri kutoka nje na ndani ya nchi, basi ni wazi timu hiyo itafanya vizuri msimu ujao utakapoanza.

“Niseme tu kuwa msimu ujao utakuwa ni mgumu lakini Simba itafanya vizuri kuliko timu nyingine kwani usajili walioufanya ni mzuri, wamechukua wachezaji wazuri kutoka timu mbalimbali ikiwemo timu yetu ya Mtibwa.

“Japo mimi siyo shabiki wa Simba lakini naona kabisa kuwa watafanya vizuri msimu ukianza, najua kombe hili hawajachukua zaidi ya misimu minne au mitano, kwa hiyo naweza kusema karata yangu ipo kwao,” alisema Kifaru.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic