July 17, 2017
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imefuta adhabu za baadhi ya waliokuwa wamefungiwa na shirikisho hilo.


Msemaji wa Simba, Haji Manara amerejea tena baada ya kufunguliwa huku Wakili msomi, Damas Ndumbaro akikosa nafa hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Abbas Tarimba amesema wao wamewafunguliwa wale ambao waliwasilisha barua kutaka hukumu zao zipitiwe.


"Wale ambao hawakuwasilisha kutaka kupitiwa upya kwa hukumu zao, tumewaambia TFF nao walifanyie kazi hilo. Kama watataka kuona inafanyika review basi haki itendeke," alisema.

Wengine walionufaika na uamuzi huo wa kamati ya nidhamu ni pamoja na Blassy kiondo ambaye in kaimu katibu mkuu wa Chama cha Soka Rukwa. James Makwinya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Rukwa na Ayubu Myaulingo ambeye ni mwenyekiti wa Chama cha Soka Rukwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV