July 17, 2017



Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Abbas Tarimba amesema wamechukua uamuzi wa kuzindoa adhabu za wadau kadhaa kwa mujibu wa sheria.

Lakini akasisitiza, adhabu ambazo hazikuwa na mashiko ni kusababisha chuki ndani ya mchezo wa soka jambo ambalo wasingelipenda.

"Lengo letu ni kuondoa chuki katika soka. Vizuri kuwa na umoja na watu wanaoshirikiana kwa ajili ya kuukuza mchezo wa soka badala ya kulalamikiana au kuchukiana," alisema Tarimba aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Yanga.

Tarimba alitangaza kufunguliwa kwa wadau kadhaa akiwemo Msemaji wa Simba, Haji Manara.

Pamoja na Manara, wengine walionufaika na uamuzi huo wa kamati ya nidhamu ni pamoja na Blassy kiondo ambaye in kaimu katibu mkuu wa Chama cha Soka Rukwa. James Makwinya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Rukwa na Ayubu Myaulingo ambeye ni mwenyekiti wa Chama cha Soka Rukwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic