July 26, 2017



Kipa Aishi Manula yupo njia panda kujiunga na timu yake mpya ya Simba iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini huku akipanga kuwapigia simu viongozi wa Azam FC ili ajue taratibu za kuingia kambini.

Manula ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara uliopangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 26, mwaka huu licha ya mwenyewe kufanya siri.

Kipa huyo, anafanya siri kutokana na mkataba wake na Azam kutarajiwa kumalizika mapema mwezi Agosti, mwaka huu.

Manula alisema kuwa yeye bado ni mchezaji halali wa Azam mwenye mkataba, hivyo ni ngumu kwake kuihama timu hiyo kutokana na kanuni za usajili kumbana.

Alisema, amepanga kuwasaliana na meneja wa timu hiyo, Philipo Alando kwa njia ya simu na kikubwa kujua taratibu za kujiunga na kambi ya Azam iliyopo Njombe ikiendelea na mechi za kirafiki.

"Niseme tu ukweli mimi bado mchezaji halali wa Azam mwenye mkataba unaoelekea ukingoni mwezi ujao, hivyo kila kitu kitajulikana baada ya mkataba kumalizika.

"Hivyo, nilichokipanga kukifanya hivi sasa ni kuwasiliana na meneja wa timu ili nijue utaratibu wa kujiunga na kambi ya Azam iliyopo Njombe.


"Ninaheshimu mkataba wangu na nisingependa nitofautiane na timu yangu,"alisema Manula kipa namba moja wa Taifa Stars.

SOURCE: CHAMPIONI.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic