July 31, 2017Baada ya kumnasa Ditram Nchimbi kutoka Mbeya City ili kuimarisha safu yake ya ushambulizi, Lipuli ya Iringa imemnasa Malimi Busungu.

Busungu amejiunga na Lipuli kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mshambuliaji huyo alikuwa hatari wakati akiwa Mgambo FC ya Tanga hadi alipojiunga Yanga.

Msimu wa kwanza akiwa Yanga alionyesha cheche lakini kuanzia katikati mambo yalibadilika mwisho akapotea mwelekeo.


Hata hivyo, Busungu aliwahi kufanya mahojiano na SALEHJEMBE na kusema angependa kuondoka Yanga na kwenda kuanza upya na anajiamini atafanya vema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV