July 28, 2017







Na Mwandishi Wetu
KASI ya awamu ya tano chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Dkt John Pombe Magufuli imezidi kutikisa kila kona ya nchi, huku wananchi wakizidi kumwagia sifa kedekede.

Ndivyo ilivyokuwa kwenye tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka linaloendelea kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, ambako vikundi karibu vyote vya ushiriki jumbe zao zilihusu ubora, ufanisi wa awamu yake ya utawala.


Mashindano hayo ambayo yalidumu kwa siku mbili na fainali kufanyika Jumanne, Julai 25, mwaka huu yalishuhudiwa Kikundi cha Mganda kutoka Luhagala kikiibuka na ushindi na kujinyakulia kombe na kitita cha shilingi laki nne. 

Aidha, kwa kiasi kikubwa kikundi hicho kilibebwa zaidi na ujumbe wa nyimbo zao katika kuisifia serikali ya Tanzania awamu ya tano kama vile inavyopambana na ufisadi, wala rushwa, kutokomeza biashara ya madawa ya kulevya huku wakimalizia na kibonzo cha HAPA KAZI TU!

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Kikundi cha Ngoma cha Ruvuma Championi, kinachoundwa na watoto chini ya umri wa miaka 18 ambako waliwakonga nyonyo watazamaji kwa umahiri wao wa kucheza ngoma za asili.



Waliondoka na kombe na fedha taslim shilingi laki tatu huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Kikundi cha Ngoma cha Kioda kinachoundwa na kina mama kutoka Luhagala. Walipewa kombe na fedha taslim laki mbili.

Mbali na fainali hizo, pia maonyesho ya ujasiriamali na utalii wa ndani ni baadhi ya shughuli zinazoendelea.




Tamasha hilo litahitimishwa Julai 30, mwaka huu kwa mashindano ya mbio za baiskeli 100 KM kutoka Wilaya ya Mbinga mpaka Songea.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic