July 27, 2017Mshambulizi Simon Msuva ametua nchini Morocco salama na kupokelewa na wenyeji wake.

Msuva amesafiri kwenda Morocco kwa ajili ya kumalizana na klabu ya Difaa Al Jadid ya nchini humo.

“Nimefika salama, kwa sasa napumzika kwanza mambo mengine yatafuatia,” alisema Msuva.


Msuva anatarajia kumalizana na kujiunga na Difaa Al Jadid ambayo msimu uliopita ilishika nafasi ya pili na itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV