July 27, 2017

Simba wameanza mazoezi ya mbinu baada ya Kocha Joseph Omog kuridhishwa na kiwango cha fitnesi.

Simba ipo kambini jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini inakojiandaa na msimu mpya.

Omog raia wa Cameroon amekiongoza kikosi chake katika mazoezi ya fitnesi kwa kipindi cha wiki na ushee.

Sasa ameingia katika mazoezi ya ufundi zaidi kuhakikisha kikosi kinakaa vizuri katika mbinu.

Baadhi ya mbinu ambazo wamekuwa wakijifunza ni pamoja na namna ya upigaji krosi, kushambulia kwa kushitukiza na mipira kirefu na mifupi.


Kazi hiyo ya maandalizi itaanza kuonekana mara ya kwanza kwenye mechi ya Simba Day itakayopigwa Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV