July 28, 2017


Kiungo mpya wa Bayern Munich, James Rodriguez ameachana na mkewe baada ya miaka sita ya ndoa. James ametua katika kikosi cha vigogo hao wa Ujerumani akitokea Real Madrid.

Daniela Ospina na mumewe walijaaliwa kupata mtoto, lakini mwanamitindo huyo ameonekana mwishoni kutoelewana na mwanasoka huyo.


Daniela ni dada wa kipa wa Arsenal, David Ospina 

Imekuwa ikielezwa kuwa James alikuwa na uhusiano na mwanamitindo mwingine aitwaye Helga Lovekaty, jambo lililosababisha kuanza kwa mfarakano ambao mwishoni wameshindwa kuurekebisha hadi wakafikia kutengana. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV