July 17, 2017

Simba imewasili nchini Afrika Kusini leo asubuhi tayari kuanza kambi.

Hata hivyo, kikosi hicho kimeondoka bila ya kocha wake wa makipa, Iddi Salim raia wa Kenya ambaye inaelezwa kabaki jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza, Simba imemchukua Mwarami lakini bado haijavunja mkataba na kocha huyo ambaye yuko katika hoteli moja jijini Dar es Salaam.

Uongozi wa Simba bado haujatangaza kumchukua rasmi Mohamed Mwarami kama kocha wa makipa lakini amekuwa akifanya mazoezi na kikosi hicho kuwanoa makipa.

Lakini habari za uhakika zinaeleza, haijavunja mkataba wake na Mkenya huyo ambaye ameendelea kubaki Dar es Salaam bila kujua hatma yake ni nini hasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV