July 19, 2017



 ya International Champions Cup kwa mwaka 2017 ilianza jana Jumanne na itafanyika katika nchi tatu tofauti ambazo ni China, Singapore na Marekani.

Michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya tano tangu kuanzishwa kwake huku kwa ufupi ikifahamika kwa jina la ICC, imekuwa ikipata nguvu na umaarufu mkubwa kila mwaka. Michuano hiyo huzikutanisha timu za mataifa tofauti kucheza mechi za kirafiki.

Baada ya kuanza jana, itaendelea hadi mwezi ujao huku kukiwa na vigogo wengi wa soka la Ulaya.

Real Madrid, Barcelona na Manchester United ni baadhi ya timu ambazo zitashiriki ambapo licha ya kwamba ni mechi za kirafiki na kutangaza biashara ya klabu hizo lakini bado zimekuwa na nguvu katika kuonyesha ubora wa vikosi vya timu husika kabla ya ligi mbalimbali kuanza.


ILIVYOANZA 
Michuano hii ilianza mwaka 2013, awali ilikuwa ni maalum kwa ajili ya Marekani hasa kwa kuwa timu kubwa za Ulaya zina wapenzi wengi kwenye taifa hilo, hivyo ziara za kwenda nchini humo ni kuwafurahisha mashabiki wao na kutangaza biashara za klabu zao ikiwemo jezi, baadaye timu zilivyoongezeka na nchi mwenyeji nazo zikaongezeka.

Kutokana na kutanuka kwa biashara ya mchezo huo, mataifa mbalimbali yamekuwa yakiandaa mechi kadhaa lakini zote zinakuwa chini ya waanzilishi walewale waliopo Marekani.

Timu mpya katika michuano ya mwaka huu ni Roma, Lyon na Arsenal, wakati hizo zikiingia zingine zilizokuwemo mwaka jana na safari hii hazimo ni Atletico Madrid, Celtic, Liverpool na Leicester City.


MASTAA KIBAO UWANJANI
Michuano ya ICC inakusanya wachezaji wengi mastaa japokuwa baadhi yao watakosekana kutokana na kuwa kwenye mapumziko. 

Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye ndiye mshindi wa Tuzo ya Ballon d'Or iliyopita, ndiye staa mwenye jina kubwa ambaye anatarajiwa kuikosa michuano hiyo kutokana na klabu yake ya Real Madrid kumpa muda wa ziada wa kupumzika.

Nyota wa Barcelona, Neymar, Luis Suarez na bwana harusi Lionel Messi, wote wanatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha timu yao kwa ajili ya mechi hizo za maandalizi.

Manchester United itakuwa na wakali wake iliowasajili hivi karibuni kama Romelu Lukaku na Victor Lindelof, pamoja na hivyo ‘bishoo’ wa timu hiyo, Paul Pogba naye yupo kikosini.

Beki aliyekuwa akiwaniwa na Manchester City kisha akatua Paris Saint-Germain, Dani Alves, naye anatarajiwa kuwemo kikosini, ambapo atakutana na timu yake ya zamani, Juventus kwa kuwa ratiba inaonyesha timu hizo zitakutana Miami mnamo Julai 26, mwaka huu.

RATIBA YA ICC
Kutokana na utofauti wa majira, michezo mingi ya Marekani itakuwa na ratiba ya kipekee ambayo inaweza kuwa ni usiku mwingi kwa baadhi ya nchi huku Watanzania wakipata burudani hiyo kupitia King’amuzi cha StarTimes kupitia chaneli zake za michezo.

King’amuzi cha StarTimes ambacho kinapatikana kwa bei rahisi, kitaonyesha michuano hiyo ‘live’ na hivyo kuwafanya Watanzania wengi kuishuhudia ambapo pia itakutanisha ‘derby’ kubwa ambazo kawaida huwa zinachezwa kwenye mataifa ya nchi husika hasa Ulaya.


DERBY ZA KIMATAIFA
Wakati imezoeleka wababe kutoka Jiji la Manchester nchini England wanakutana kwenye jiji lao hilo katika michezo ya Premier League, safari hii watakutana ndani ya Marekani katika Manchester Derby.

Timu hizo ni Manchester United na Manchester City ambazo zitakipiga kwenye Uwanja wa NRG pande za Houston ndani ya Texas, alfajiri ya kuamkia Ijumaa ya keshokutwa.

Derby nyingine ni ile ya alfajiri ya Julai 29, 2017 kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona, hawa ni wababe wa Hispania katika La Liga, siku hiyo watakutana kwenye Uwanja wa Hard Rock mitaa ya Miami Gardens ndani ya Florida.


ALIYESHINDA MWAKA JANA
Kila kituo huwa kinakuwa na mshindi wake kwa kuwa timu hazitakiwi kusafiri umbali mrefu wa kuwachosha wachezaji ili wampate bingwa wa pamoja.

Kwa mwaka jana bingwa alipatikana katika sehemu mbili tu kwa kuwa upande wa China mchezo kati ya Manchester City na Manchester United uliahirishwa baada ya uwanja uliotakiwa kutumika kutokuwa katika ubora mzuri baada ya mvua kubwa kunyesha.

Juventus walikuwa mabingwa upande wa Australia kwa kuifungwa Melbourne Victory kwa penalti wakati PSG walikuwa mabingwa upande wa Marekani mbele ya Liverpool, Chelsea, Barcelona na Real Madrid.

MAKUNDI INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP 2017

Marekani
Ligi
Paris Saint-Germain Ligue 1
Juventus Serie A
Roma Serie A
Barcelona La Liga
Real Madrid La Liga
Manchester City Premier 
Manchester United Premier 
Tottenham Hotspur London


CHINA
Ligi
Bayern Munich Bundesliga
Borussia Dortmund Bundesliga
Inter Milan Serie A
Milan Serie A
Olympique Lyon Ligue 1
Arsenal Premier League


SINGAPORE
Ligi 
Bayern Munich Bundesliga
Inter Milan Serie A
Chelsea Premier League


RATIBA YA UKANDA WA AMERIKA
Julai 20, 2017
Roma Vs PSG 10:00 Alfajiri

Julai 21, 2017
Man United Vs Man City 10:30 Alfajiri

Julai 23, 2017
Juventus Vs Barcelona 07:00 Usiku
PSG Vs  Tottenham 09:00 Usiku

Julai 24, 2017
Real Madrid Vs Man United 06: 00 Usiku

Julai 26, 2017
Tottenham Vs Roma  09:00 Usiku

Julai 27, 2017
Barcelona Vs Man United 08:30 Usiku
PSG Vs Juventus 09:30 Usiku
Man City Vs Real Madrid 12:00 Asubuhi


Julai 30, 2017
Man City Vs  Tottenham 07:00 Usiku
Real Madrid Vs Barcelona 08:30 Usiku

Roma Vs Juventus 5:00 Usiku

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic