July 19, 2017




Kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya SportPesa leo imetoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwa kutoa baraka na kufanikisha ziara ya klabu ya Everton ya Uingereza.


Pamoja na hivyo, alimshukuru Makamu wa Rais mama Samia Suluhu kwa kushirikiana nao mwanzo hadi mwisho wakati wa ziara hiyo hadi alipokuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo.


Waandishi wa habari, nao walipata shukurani kubwa kutokana na ushiriki wao kabla ya ujio wa Everton, walipofika na hata baada ya kuondoka.

Tarimba amesema wamejifunza mambo mengi yakiwemo makosa kama wanadamu na wamejipanga kurekebisha kila walipoteleza kwa lengo la kufanya mambo yawe vizuri.


Kauli hiyo, imetolewa ikiwa ni siku chache tangu mechi ya kirafiki kati ya Gor Mahia na Everton ichezwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Everton iliyoongozwa na nahodha wa zamani wa Manchester United ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za kampuni hiyo, Masaki jijini Dar es Salaam Mkurugenzi, Maendeleo na Uendeleshaji, Tarimba Abbasi alisema serikali imesaidia mengi katika ziara hiyo.

Tarimba alisema, wanalishukuru Jeshi la Polisi, Bodi ya Utalii Tanzania (TBB), Uhamiaji, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo chini ya waziri wake, Harrison Mwakyembe kwa kufanikisha ziara huyo.

“SportPesa tuchukue nafasi hii kuzipongeza wizara mbalimbali hapa nchini zilizoshiriki kufanikisha ziara ya Everton, kiukweli kabisa ziara hii imeweza kuitangaza vema Tanzania.

“Pongezi nyingi ziende rais wetu Magufuli, Mwakyembe mwenye dhamana ya michezo bila kuzisahau taasisi mbalimbali ikiwemo bodi ya Utalii, Uhamiaji na TFF,” alisema Tarimba.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic