Huku michuano ya International Champions Cup 2017, ikiendelea kutikisa kwa kasi ya hali ya juu, timu za England zimeonekana kutikisa.
Michuano hiyo imeonekana kung'ara zaidi msimu huu huku Watanzania wakifaidi utamu wake kupitia king'amuzi cha StarTimes kinachorusha mubasharaa matangazo ya mechi hizo.
Katika michuano hiyo mikubwa ya kujiandaa na msimu mpya ambayo inaonyeshwa mubashara na Startimes, imekuwa mikubwa zaidi kwa timu zote zinazojiandaa na msimu mpya wa ligi.
Katika michuano hiyo ambayo inafanyika kwenye nchi za Marekani, China na Singapore, timu za England zinazoshiriki ni tano na zote zimekuwa zikionyesha kiwango cha juu.
Usiku wa kuamkia leo, kulikuwa na mchezo mgumu sana na wa heshima, wakati Manchester United walipokuwa wakiwakaribisha Real Madrid ya Hispania kwenye mchezo mkali uliokuwa unasubiriwa na mashabiki kwa hamu kubwa.
Hadi sasa matokeo yanaonyesha kuwa Arsenal ambao walichapwa na Chelsea juzi kwa mabao 3-0, walifanikiwa awali kuwachapa Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich kwa penalti 3-2.
Julai 20, Man Utd walifanikiwa kuwachapa Man City mabao 2-0.
Huku Julai 22, Tottenham wakiwachapa mabingwa wa Ufaransa, PSG kwa mabao 4-2.
Kama Madrid walichapwa na Manchester United basi timu za England zitakuwa zimewachapa mabingwa wa mataifa manne makubwa.
Hii inaonyesha kuwa pamoja na timu zote kujiandaa vyema, lakini timu za England zimekuwa mahiri sana kwenye michuano hii.
Matokeo ya ICC hadi sasa…
Julai 18 Milan 1-3 Borussia Dortmund
Julai 19 Bayern Munich 1-1 (2-3 penalti) Arsenal
Julai 19 Roma 1-1 (3-5 penalti) PSG
Julai 20 Man Utd 2-0 Man City
Julai 22 Barcelona 2-1 Juventus
Julai 22 Tottenham 4-2 PSG
Julai 22 Bayern Munich 0-4 Milan
Julai 24 Madrid 1-2 Man United
0 COMMENTS:
Post a Comment