July 31, 2017




Sakata la Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia limeingia katika sura mpya kwa kuwa sasa Idara ya Uhamiaji Tanzania, imeamua kuchukua vipimo vya vinasaba vyake.

Karia sasa ni mgombea Urais wa TFF, uchaguzi ambao utafanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

Ally Mtanga, Mkuu wa Mawasiliano Idara ya Uhamiaji Tanzania

“Tutafanya vipimo vya vinasaba, kuna misingi miwili ya kuchambua.

“Kuzaliwa kwa haki ya ardhi, msingi wa pili ni haki ya damu. Haitoshi mtu kuzaliwa, lazima awe na mzazi mmoja aliyekuwa raia wa pale na ndiyo tunaangalia vinasaba.


“Kwa kuwa anaemia mzazi wake mmoja ni mzaliwa wa serikali. Hivyo atapimwa kuangalia kama ni mama yake mzazi,” alisema.

Karia aliwekewa pingamizi wakati wa mapingamizi ya uchaguzi lakini alipita kwenye usaili baada ya mtoa pingamizi kutowasilisha ushahidi wa kutosha.

Lakini Karia mwenye alikiri kuwa na asili ya Tanzania kwa kuwa mama yake ni Mtanzania na baba yake ni Msomali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic