July 28, 2017


Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula ‘Mzazi’ kwa sasa yupo hoi kitandani akijiuguza kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ngozi.

Mwaisabula amewahi kuinoa Yanga miaka ya 1990 ikiwa na wachezaji nyota akiwemo Deo Lucas, huku akiwa na heshima kubwa katika soka la Tanzania.

Mwaisabula amesema kuwa kwa sasa hali yake siyo nzuri kutoka na kusumbuliwa na ugonjwa huo ambapo amekuwa mtu wa kukaa nyumbani tofauti na awali.

“Hali yangu siyo nzuri, nasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi, ni tatizo la muda mrefu ambalo limekuwa likinisumbua ila kwa sasa hali imekuwa tofauti na awali.

“Nipo nyumbani najiuguza kwa sababu wataalum ndiyo waliosema na hata ukiiona ngozi yangu kwa sasa haipo kawaida, shughuli zangu siwezi kufanya naomba wadau waniombee ili nirejea katika hali ya kawaida,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV