August 28, 2017




Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya mabadiliko kidogo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kama ifuatavyo.

Michezo ambayo imefanyiwa mabadiliko ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea; Azam FC na Simba, Njombe Mji na  Young Africans; Mtibwa Sugar na Mwadui FC ambayo sasa itachezwa Septemba 6, 2017.

Pia tarehe hiyo ya Septemba 6, mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Lipuli na Stand United; Singida United na Mbao; Kagera Sugar na Ruvu Shooting wakati Mbeya City na Ndanda FC .

Michezo mingine ambayo imesogezwa hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na Kagera Sugar wakati Mbao na Tanzania Prisons utachezwa Septemba 21, mwaka huu.

Kadhalika mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United.

Tarehe hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.


Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba.

2 COMMENTS:

  1. TFF hawajawa tayari kuwa na LIGI isiyokuwa na viraka. Ni jambo la ajabu sana kuahirisha mechi kwa sababu yoyote ile iwayo timu zimesajili wachezaji zaidi ya 25 inakuwaje ziondokewe na wachezaji ndipo ligi iahirishwe? Haya ndiyo yanayodumaza vipaji na kuua soka Tanzania. Na mwisho wa siku yanapelekea matokeo ya mechi kupangwa.
    sijaona tofauti ya TFF hii na iliyopita ni TFF ileile na sitarajii kama kutakuwa na mapya. Kwa akili "zetu" itasemwa tuwape muda ilhali pale hakuna mgeni.

    ReplyDelete
  2. Tulishasema wajumbe Wa tff walishamrudisha Malinzi indirectly. Hakuna mabadiliko yoyote, kalia hamna kitu pale.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic