Mshambuliaji Diego Costa hatimaye ameonekana kwenye uwanja wa soka kwa mara nyingine baada ya kujichimbia nyumbani kwao Lagarto Mashariki mea Brazil.
Costa yuko kwenye mgogoro mkubwa na kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye alimtumia SMS akimueleza hamtaki.
Baada ya hapo, alimshuka katika timu ya akiba kufanya nayo mazoezi mambo alilokataa na kuamua kwenda kuishi Lagarto alikozaliwa.
Hata hivyo, Costa anayeichezea timu ya taifa ya Hispania, ameibuka kwenye mmoja wa viwanja katika eneo hilo alilozaliwa baada ya kukaribishwa kama mgeni rasmi.
Alialikwa kuwa mgeni rasmi katika mechi kati ya Confianca dhidi ya CSA iliyopigwa katika mji mdogo wa Aracaju na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki waliomshangilia kwa nguvu.
0 COMMENTS:
Post a Comment