August 24, 2017




Manchester United imethibitisha kumsajili kwa mara nyingine mshambulizi Zlatan Ibrahimovic.

Zlatan aliumia na kuamua kuondoka United, lakini imethibitishwa kuwa amerejea tena Old Trafford na sasa ni shetani mwekundu tena.



Wakati wa msimu wa 2016-17, mshambulizi huyo raia wa Sweden aliichezea Man United mechi 46 na kufunga mabao 28 kabla ya kuumia.


Taarifa zinaeleza, safari hii Man United watampa jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Wayne Rooney aliyehamia Everton.


Hivi karibuni, baada ya kupona, Zlatan alirejea katika viwanja vya mazoezi vya Man United na kuonekana kuwa sasa yuko fiti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic