August 16, 2017


Kiungo kinda mwenye kasi wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele inaonekana safari yake ya kwenda Barcelona imeiva.

Barcelona imekubali kumwaga kitita cha pauni million 90 ili kumnasa.

Leo, ameonekana Dembele akiwa na rafiki na ndugu zake wakimsaidia kuweka vitu kadhaa kwenye gari lake kama mtu anayehama nyumba.


Ingawa hakuna kati ya Barcelona au Dortmund aliyesema kwamba Dembele yu tayari kuondoka, tukio hilo ni dalili tosha Dembele anakwenda Barcelona kuziba pengo la Neymar ambaye amejiunga na PSG ya Ufaransa kwa dau kubwa la pauni milioni 198.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic