August 16, 2017


Kampuni maarufu ya ving’amuzi ya StarTimes imezindua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Soka ya Ujerumani ya Bundesliga.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo na kuongozwa na Makamu Rais wa StarsTimes Tanzania,Zuhura Hanif.


Katika uzinduzi huo, StarTimes walieleza ubora wa ligi hiyo na namna Watanzania wanavyoweza kushuhudia mechi kupitia StarTimes.

Mechi ya ufunguzi itakuwa keshokutwa Ijumaa wakati mabingwa Bayern Munich wakiwavaa Bayer Leverkusen katika dimba la Allianz Arena jijinim Munich.

StarTimes wamekuwa wakionyesha ligi hiyo kwa msimu wa tatu mfululizo.

Bundesliga imekuwa ligi bora zaidi kwa takwimu nyingi uwanjani na hata watazamaji na imeendelea kufanya vizuri kwa misimu mingi zaidi.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic