August 31, 2017


LWANDAMINA AKIWA NDANI YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (JNIA) JIJINI DAR ES SALAAM, LEO.
Hatimaye kilichomuondoa Kocha wa Yanga, George Lwandamina na kurejea kwao Zambia kimejulikana.

Lwandamina ameondoka leo kurejea kwao Zambia na awali ilielezwa ni matatizo ya kifamilia, lakini yeye mwenye ameiambia SALEHJEMBE kwamba amepata msiba mkubwa.

"Nimepata msiba mkubwa, nimempoteza baba yangu mzazi siku chache zilizopita. Sasa narejea nyumbani kwa ajili ya mazishi," alisema.
Kocha huyo mtaratibu amesema atarejea na kujiunga na kikosi chake mara tu atakapomaliza suala hilo la mazishi ya mzazi wake.

BLOG YA SALEHJEMBE, INATOA POLE KWA KOCHA LWANDAMINA NA KUMUOMBEA AWE NA NGUVU NA KULIMALIZA SUALA HILO KATIKA WAKATI HUU MGUMU.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic