August 5, 2017



Ungeweza kufikiri baada ya pacha wake, Haruna Niyonzima kuondoka, kiungo rasta wa Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko angeweza kuwa na hofu kubwa.

Lakini mambo ni tofauti kabisa, ameonyesha kujiamini zaidi na ametamba kikosi chao hivi sasa kipo fiti kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo, ameitoa mara baada ya kumaliza kambi ya mkoani Morogoro waliyoiweka kwa muda wa wiki mbili kujiandaa na ligi kuu iliyopangwa kuanza Agosti 26, mwaka huu. Pia kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 23, mwaka huu.

Kiungo huyo, wiki hii alijiunga na kambi hiyo akitokea kwao Zimbabwe alipokwenda muda mfupi baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo.

Kamusoko alisema anafurahia kuona kila mchezaji akiwa fiti baada ya kumaliza mazoezi ya fitinesi kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam, jana.

Kamusoko alisema, wamepanga kuendelea kulitetea tena taji lao la ligi kuu walilolichukua kwa misimu mitatu mfululizo chini ya kocha wao wa zamani Hans van Der Pluijm na baadaye Mzambia, George Lwandamina.

"Nawapongeza viongozi kwa kufanikisha kambi hii ya wiki mbili ya pamoja ya mazoezi ya fitinesi tuliyoiweka huku Morogoro.


"Kiukweli kabisa ukiangalia kila mchezaji unamuona yupo fiti kwa ajili ya mapambano, hivyo tunawaahidi mashabiki wetu kufanya vizuri katika msimu ujao,” alisema Kamusoko.

4 COMMENTS:

  1. Kuna kitu hakipo sawa,Simba imempoteza Ajib lakini haijaweweseka kama yanga inavyoweweseka juu ya Niyonzima,inaonekana huko yanga kuna ratiba maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kumzungumzia Niyonzima jambo linalodhihirisha kuwa yanga imepata pigo sana kumpoteza Niyonzima kuliko Simba kumpoteza Ajib.

    Kwa nini msijipange na kumsahau Niyo kama Simba ilivyofunga mjadala wa Ajib na ikamsahau?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe peke yako ndio umefunga, wako wanaotoa povu kwa AJibu mpaka leo,au wee huoni anavyotukanwa?

      Delete
  2. Hizi habari zote zinatengenezwa na waandishi. Nina uhakika Kamusoko asingemzungumzia Niyonzima kama Mwandishi asingemfuata na kumuuliza.

    ReplyDelete
  3. tatizo letu watanzania huwa hatupendi kusema ukweli panapoonekana kuna ukweli.
    bado nasema Niyonzima alikuwa mchezaji muhimu sana ndani ya yanga na kuondoka kwake kumeleta pengo wewe unaebisha acha kuiweka akili yako katika giza.

    Niyonzima alikuwa nafasi gani na ajibu je???
    sasa ww unaesema si chochote majibu utayapata.
    tupende kuwa wakweli na sio kujikaza ila cha msingi zaidi ni kumuombea azidi kuimarisha kiwango chake kwani mwisho wa siku kila mtu anatafuta pesa na amani katika maisha.

    nakupongezaNiyonzima kutimiza furaha yako nakupongeza ajibu kutimiza lengo lako kwani maisha ni furaha na amani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic