Wakati ulifikiri Masau Bwire angepata shida sana baada ya timu yake ya Ruvu Shooting kupokea kipigo cha mabao 7-0 kutoka kwa Simba, basi ulijidanganya.
Kipigo hicho kinabaki kama sehemu ya uchungu uliopita kwa Masau lakini msemaji huyo wa Ruvu Shooting, pia alionja upande wa utamu wa kipigo hicho.
MOJA:
Kwanza alianza kwa kushangiliwa ile mbaya na mashabiki wa Simba wakati mechi ikiendelea na wengine waliimba jina lake "Masau, Masau, Masau", jambo ambalo hata mashabiki wa Ruvu Shooting hawajawahi kulifanya.
MBILI:
Mashabiki wa Simba, waliamua kwenda kumpokea nje wakati akitoka kwenda kupanda basi la timu yake aondoke, wakapiga naye picha huenda hata kuliko wachezaji wao wa Simba.
Hakuna mchezaji wa Ruvu Shooting aliyewahi kupata shangwe kama alizozipata Masau.
TATU:
Hii ndiyo funga kazi, pamoja na yote, konda mmoja wa daladala na dereva wake ambao ni mashabiki wa Simba, waliamua Masau asilipe nauli.
Kisa cha wao kuamua asilipe nauli ni kwa kuwa wanaona ni mtu mwenye maumivu na wao wameamua kumpa pole.
"Kila nikipita mtaani, basi huku naitwa, kule naitwa na mimi naona ndiyo ushabiki wenyewe."
"Lakini kuna daladala nilipanda, kona na dereva wakaona nisilipe nauli. Wao ni mashabiki wa Simba, walitaka kunipa pole kutokana na kile kipigo," anasema Masau.
0 COMMENTS:
Post a Comment